Sera ya faragha

Utangulizi 

Kampuni zinazoshiriki katika Mpango wa Usawa katika Urejeshaji zimechukua hatua nchini na kimataifa kukabiliana na athari za kijamii za sekta isiyo rasmi ya taka. 

Kama sehemu ya mchakato wa kuratibu Mpango wa Usawa katika Urejeshaji, Tearfund inapangisha tovuti hii. Kwa madhumuni ya sera hii, maneno ‘sisi’ na ‘-etu’ yanarejelea Tearfund. Ambapo Tearfund imetajwa, inajumuisha Tearfund Trading Limited, kampuni yetu ya biashara.

Tearfund ni shirika la misaada na maendeleo la Kikristo lililosajiliwa Uingereza na Wales (nambari 265464) na Scotland (SCO 37624). Kampuni yetu ni nambari 994339 na ofisi yetu iliyosajiliwa ni 100 Church Road, Teddington, TW11 8QE.

Tearfund imejitolea kulinda data yako kwa kutii Sheria ya Ulinzi wa Data ya 2018, sheria ya UK GDPR na Kanuni za Faragha katika Mawasiliano ya Kielektroniki, na kuheshimu haki za wamiliki wa data. Faragha na utulivu wako wa akili ni muhimu kwetu. Huwa tunakusanya data kutoka kwa watu kwa madhumuni mahususi pekee na madhumuni hayo yakishatekelezwa, hatuhifadhi data hiyo.

Sera hii ya Faragha inaeleza sababu na jinsi tunavyokusanya na kutumia taarifa zako binafsi, jinsi tunavyolinda na kushiriki taarifa hizo na hatua za kuchukua endapo una swali au shaka kuhusu matumizi haya. Sera hii ya Faragha inatumika tu kwa taarifa binafsi zinazochakatwa kuhusiana na Mpango wa Usawa katika Urejeshaji.

Orodha kamili ya mashirika ambayo ni sehemu ya Mpango wa Usawa katika Urejeshaji inapatikana kwenye ukurasa wa kwanza.

Taarifa tunazokusanya

Huwa tunakusanya data kwenye tovuti hii kwa sababu kadhaa, hasa kukupatia taarifa faafu na bora zaidi kuhusiana na Mpango wa Usawa katika Urejeshaji. Tunafanya hivi kwa kukusanya data binafsi unayotupatia mtandaoni na kwa kukusanya na kuchambua data kutoka kwenye tovuti yetu. Katika sehemu fulani za tovuti yetu, kama vile fomu, barua pepe, maoni, kura na majibu ya utafiti, unaweza kutupatia data binafsi. Data ya matumizi ya tovuti hukusanywa kwa kutumia vidakuzi.

Taarifa tunazokusanya sanasana zinaweza kujumuisha:

  • Maelezo ya kibinafsi kama vile jina lako, 
  • Maelezo ya mawasiliano kama vile anwani yako ya barua pepe na shirika unalowakilisha
  • Mapendeleo ya mawasiliano

Sababu ya kuzikusanya

Taarifa tunazokusanya hutusaidia kukutumia taarifa na maelezo kuhusu Mpango wa Usawa katika Urejeshaji.

Tunatumia taarifa binafsi unazotupatia kwa madhumuni ambayo umeitoa na kwa madhumuni mengine yoyote ambayo umetupatia ruhusa kuzitumia.

Mpango wa Usawa katika Urejeshaji unaweza kutumia taarifa zako binafsi kwa njia zifuatazo:

  • Kukufunza na kukufahamisha kuhusu Mpango wa Usawa katika Urejeshaji na kazi ya mpango huu
  • Kutangaza matukio na nyenzo za mafunzo na utetezi ambazo zinawiana na Mpango wa Usawa katika Urejeshaji. 
  • Kujibu maoni au maswali yako
  • Au kwa madhumuni mengine yoyote ambayo yatatajwa mahususi na Mpango wa Usawa katika Urejeshaji wakati wa kukusanya taarifa zako binafsi.

Una haki ya kutuomba tusichakate taarifa zako binafsi kwa madhumuni ya utangazaji. Tutakujulisha (kabla ya kukusanya data yako) kama tunanuia kutumia data yako kwa madhumuni kama hayo. Unaweza kutumia haki yako ya kuzuia uchakataji kama huo kwa kuteua visanduku fulani kwenye fomu tunazotumia kukusanya data yako. Unaweza pia kutumia haki hiyo wakati wowote kwa kuwasiliana nasi.

Msingi wetu wa kuzichakata

Sheria za kulinda data zinahitaji tuwe na msingi mwafaka wa kisheria wa uchakataji wa taarifa zako binafsi. Tunapochakata data yako binafsi tunategemea:

  • Ambapo umetupatia idhini ya kuwasiliana nawe au kuhifadhi taarifa zako.
  • Ambapo ni kwa maslahi yetu halali kufanya hivyo kama ilivyoelezwa hapo juu.
  • Ambapo tunategemea maslahi yetu halali kuchakata data yako (ikiwa ni pamoja na kuwasiliana nawe), huwa tunafanya hivyo tu baada ya kuzingatia jinsi inavyoweza kukuathiri wewe na haki zako na kuweka hili kwenye mizani na haja yetu ya kuwasiliana nawe.

Jinsi zinavyokusanywa

Tearfund hukusanya taarifa binafsi na nyeti moja kwa moja kutoka kwako kuhusiana na Mpango wa Usawa katika Urejeshaji. Sanasana, unatoa data kwa Tearfund kwa kujisajili ili kuonyesha nia kwenye tovuti ya Mpango wa Usawa katika Urejeshaji, kutoa maelezo kwenye simu au barua pepe au kwa kushiriki katika mojawapo ya hafla zetu ambapo unatoa au kujaza taarifa zako binafsi kwa hiari.

Baadhi ya taarifa zako binafsi pia zinaweza kukusanywa kiotomatiki kama ilivyoelezwa hapo chini.

Vidakuzi

Tunatumia vidakuzi kukusanya data. Kidakuzi ni faili ya matini inayotumwa na tovuti na kuhifadhiwa kwenye diski kuu ya kompyuta yako na kivinjari chako cha wavuti, ili kukusanya data ya kawaida ya kumbukumbu za intaneti na maelezo ya mienendo ya anayetembelea tovuti hiyo. Vivinjari vingi hukuruhusu kuzima utendakazi wa vidakuzi, hata hivyo ukichagua kufanya hivi huenda usiweze kufikia sehemu fulani za tovuti. Isipokuwa uwe umerekebisha mpangilio wa kivinjari chako ili kikatae vidakuzi, mfumo wetu utatoa vidakuzi punde unapotembelea tovuti yetu.

Zaidi ya taarifa unazotoa mahususi, vidakuzi vinaweza kutumiwa kukusanya taarifa za jinsi unavyotembelea tovuti yetu (kwa mfano, lakini si tu, data ya trafiki ya mtandaoni, data ya mahali, maelezo ya kifaa, data ya mawasiliano, tarehe na wakati unapotembelea tovuti na kurasa unazotazama). Data ya aina hii hukusanywa kwa ujumla na haimtambulishi mtu. Data ya aina hii hutusaidia kuelewa jinsi watu wanavyotumia tovuti yetu ili tuweze kukidhi mahitaji yako vyema zaidi katika usanidi wa tovuti katika siku zijazo.

Tunaweza pia kutumia data hii iliyokusanywa kiotomatiki kwa madhumuni yafuatayo:

  • kurekebisha maudhui yaliyo kwenye tovuti kulingana na mahitaji ya sasa na ya baadaye ya wanaoitembelea
  • kuchakata maombi au miamala yoyote unayofanya
  • kwa ajili ya usimamizi na uchambuzi wa ndani

Matumizi ya vidakuzi ni jambo la kawaida katika tasnia kwenye tovuti nyingi kubwa.  Tovuti mbalimbali zinatoa maelezo ya kina kuhusu vidakuzi, ikiwa ni pamoja na AboutCookies.org na AllAboutCookies.org.  Ikiwa hutaki kupokea vidakuzi unaweza  kurekebisha kivinjari chako cha wavuti kwa urahisi ili kikatae vidakuzi au kikujulishe unapopokea kidakuzi kipya.

Ukijisali nasi au ukiendelea kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi.

Matumizi ya Anwani za Itifaki Wavuti (IP)

Huwa tunakusanya anwani za itifaki wavuti (IP) ili kupata taarifa zilizojumlishwa kuhusu matumizi ya tovuti hii. Anwani ya IP ni nambari ambayo seva ya wavuti hupatia kompyuta yako unapokuwa mtandaoni. Tuna seva inayorekodi anwani ya IP ya kompyuta yako unapotembelea tovuti yetu.

Huwa tunatumia maelezo tunayopata kutokana na kufuatilia anwani za IP kwa ujumla, kwa mfano kujua idadi ya watu waliotembelea sehemu fulani ya tovuti yetu, wala si kufuatilia anwani mahususi za IP ili kumtambua mtumiaji mahususi. Hata hivyo, tunaweza kutumia maelezo hayo kumtambua mtumiaji ikiwa tunahisi kwamba kunayo/kuna uwezekano wa kuwepo kwa masuala ya usalama na/au ulinzi au kutimiza matakwa ya sheria.

Wahusika wengine

Tearfund haiuzi, kukodisha au kufichua taarifa zozote binafsi kwa wahusika wengine kwa madhumuni yao ya utangazaji.

Tearfund hainunui wala kutumia taarifa binafsi zinazotolewa na wahusika wengine. Hatutafikia wala kutumia taarifa zozote binafsi ambazo umeshiriki hapo awali moja kwa moja na mashirika wanachama wa Mpango wa Usawa katika Urejeshaji isipokuwa uwe umetoa idhini mahususi.

Taarifa binafsi tunazokusanya kutoka kwako zitahifadhiwa katika hifadhi data kuu ya Mpango wa Usawa katika Urejeshaji. Hifadhi data hii inaweza kufikiwa na wafanyakazi mahususi wa mashirika wanachama wa Mpango wa Usawa katika Urejeshaji.  Utapokea mawasiliano (ukikubali kuyapokea) kutoka moja ya mashirika wanachama wa Mpango wa Usawa katika Urejeshaji (kawaida ni kwamba Tearfund itawasiliana nawe isipokuwa kama tayari umejisajili kupokea taarifa kutoka shirika lingine kati ya wanachama wa Mpango wa Usawa katika Urejeshaji) kuhusiana na Mpango huu tu. Hutapokea mawasiliano ya matangazo kutoka kwa mashirika wanachama wa Mpango wa Usawa katika Urejeshaji isipokuwa uwe umetoa idhini mahususi ya kuyapokea.

Tearfund pia inaweza kushiriki taarifa zako:

  • Na wahusika wengine ambao wanatoa huduma za kusaidia Mpango wa Usawa katika Urejeshaji. Kwa mfano, kwa programu ya kutuma barua pepe kama vile Mailchimp kwa kusudi la kutuma taarifa au;
  • Kulingana na matakwa ya sheria.  

Katika hali hizi chache, Tearfund itachukua hatua zote zinazofaa kuhakikisha kwamba data yako i salama na inatumika tu kwa sababu ile moja iliyonuiwa. Mikataba mwafaka ya usiri na matumizi ipo baina ya wanachama wa Mpango wa Usawa katika Urejeshaji ili kuhakikisha usalama na faragha ya data.

Kuheshimu faragha yako

Data tunayokusanya kutoka kwako inaweza kuhamishiwa, na kuhifadhiwa, mahali palipo nje ya Eneo la Kiuchumi la Ulaya (“EEA”) ambapo ulinzi unaofaa umewekwa. Inaweza pia kuchakatwa na wafanyakazi wa Tearfund walio nje ya eneo la EEA, mwanachama mwingine wa Mpango au mmoja wa watoa huduma wetu. Wafanyakazi hao wanaweza kuwa wanahusika na utoaji wa huduma saidizi, pamoja na mengineyo. Kwa kutoa data yako ya kibinafsi, unakubali uhamishaji, kuhifadhi au uchakataji huu. Tearfund itachukua hatua zote zinazohitajika kama inavyofaa kuhakikisha kwamba data yako inashughulikiwa kwa usalama na kulingana na sera hii ya faragha.

Tearfund inajitahidi kuhakikisha kwamba data tuliyo nayo kukuhusu ni sahihi. Endapo utaona makosa yoyote au ikiwa hutaki tena kupokea taarifa kutoka kwetu, tafadhali wasiliana nasi.

Salama salimini

Tunadumisha kiwango cha juu cha usalama halisi na wa kielektroniki katika ukusanyaji, kuhifadhi na ufichuzi wa taarifa zako. Tunachukua hatua zinazofaa kuhakikisha kwamba data yoyote tuliyo nayo kukuhusu inalindwa.

Ingawa tunafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba taarifa zinazotumwa kwetu zinatumwa kwa usalama, hatuwezi kutoa hakikisho la usalama wa taarifa zinazotumwa kwetu kupitia intaneti. Unapotutumia taarifa kupitia intaneti, unafanya hivyo kwa kuwajibikia hatari iliyopo mwenyewe.

Tutahifadhi data yako binafsi kwa muda ambao tunaonelea unahitajika kutekeleza kila shughuli tu. Tunazingatia wajibu wa kisheria, masuala ya uhasibu na kodi pamoja na kuzingatia kinachofaa kwa shughuli husika. Tunatekeleza haya kulingana na sera yetu ya kuhifadhi data.

Jinsi ya kuwasiliana nasi

Tearfund huweka na kuchakata taarifa binafsi kulingana na Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data au sheria nyingine yoyote ya ulinzi wa data inayotumika na imesajiliwa katika Ofisi ya Kamishna wa Data, kama mdhibiti wa data.

Ikiwa una maswali yoyote kuhusu jinsi taarifa zako zinavyoshughulikwa au una maswali kuhusu sera hii ya faragha, tafadhali wasiliana nasi kupitia info@tearfund.org au unaweza kutuandikia kupitia:

Data Protection Officer

Tearfund
100 Church Road
Teddington
UK
TW11 8QE

Haki zako

Una haki ya:

  • kutuomba tufute data yako binafsi;
  • kuweka mipaka ya uchakataji wa data yako binafsi;
  • kupinga kuchakatwa kwa data yako ya kibinafsi, kwa mfano pale ambapo tumetegemea maslahi halali ili kuchakata data yako; 
  • kukataa michakato inayofanya uamuzi kiotomatiki na uainishaji;
  • kuhamisha data binafsi (yaani kuomba data yako itoloewe kwa shirika lingine kielektroniki);
  • kupata taarifa zako. Una haki ya kuomba maelezo ya taarifa tulizo nazo kukuhusu. Tutajibu ndani ya muda wa mwezi mmoja baada ya kupokea ombi lako.
  • kutuomba tusahihishe taarifa binafsi ambazo unaonelea si sahihi. Pia una haki ya kutuomba tukamilishe taarifa unazoonelea si kamili.

Unaweza kutumia haki hizi wakati wowote kwa kutuandikia kupitia:

Data Protection Officer
Tearfund
100 Church Road
Teddington
UK
TW11 8QE

kututumia barua pepe kupitia: info@tearfund.org

kutupigia simu kupitia nambari +44 20 3906 3906

Kwa maelezo zaidi kuhusu haki zako chini ya Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data unaweza kutembelea tovuti ya Ofisi ya Kamishna wa Data https://ico.org.uk/

Mabadiliko katika taarifa ya Tearfund kuhusu faragha

Sera hii ilibadilishwa mwisho Oktoba 2022. Mara kwa mara tunaweza kurekebisha taarifa hii ili kuisasisha na kuhakikisha inafaa. Tafadhali hakikisha unairejelea mara kwa mara ili uone mabadiliko yaliyofanywa.

Malalamiko

Ikiwa una maswali yoyote au ungependa kuwasilisha malalamiko, unaweza kufanya hivyo kwa njia zifuatazo:

Kutupigia simu kupitia: +44 20 3906 3906

Kututumia barua pepe kupitia: info@tearfund.org

Kutuandikia kupitia:

Data Protection Officer
Tearfund
100 Church Road
Teddington
TW11 8QE

Una haki pia ya kutuma malalamiko kuhusu matumizi ya data yako binafsi kwa Ofisi ya Kamishna wa Data (ICO), ambayo ni mamlaka ya ulinzi wa data Uingereza. Unaweza kufanya hivyo kwa kupiga nambari ya usaidizi ya ICO au kwa kutembelea tovuti ya ICO. Maelezo zaidi yanapatikana https://ico.org.uk/concerns