Juhudi za Kuheshimu Haki za Binadamu katika Urejeshaji

Mpango wa Usawa katika Urejeshaji unaleta pamoja biashara kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba haki za wafanyakazi katika sekta isiyo rasmi ya taka zinaheshimiwa na wajibu wao muhimu katika minyororo ya thamani ya uchumi rejeshi unatambuliwa. 

Kanuni za Usawa katika Urejeshaji

Kanuni za Usawa katika Urejeshaji, ambazo zinazingatia mtazamo wa wamiliki wa haki, zinatumia matakwa na majukumu yaliyoelezwa katika Mwongozo wa Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Haki za Binadamu katika sekta isiyo rasmi ya taka.

Kampuni zinazoshiriki katika mpango huu zimeshikamana kuunga mkono Taarifa hii ya Uzinduzi na Kanuni za Usawa katika Urejeshaji, ili kudhihirisha kujitolea kwetu kwa suala hili na kuhimiza kwamba Kanuni za Usawa katika Urejeshajii zikubaliwe kwa upana zaidi na zitekelezwe kwa dharura.  

Tutafanya yafuatayo:  

  • kuendeleza na kutumia kanuni hizi katika minyororo yetu ya thamani, kwa ushirikiano na mashirika ya wakusanyaji taka
  • kutoa ripoti ya hatua tulizopiga kila mwaka
  • kuwahimiza wengine wajiunge na Mpango wa Usawa katika Urejeshaji

 

Washiriki Waanzilishi

Mratibu

Sekretarieti

Onyesha Nia

Tunabuni utaratibu wa kuomba kujiunga na mpango huu na tungependa kukufahamisha jinsi mchakato huo unavyoendelea.

Onyesha Nia